Mh Membe atoa somo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Tusiime

Mh Membe atoa somo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Tusiime

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Tusiime kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambapo wanafunzi hao walipata nafasi ya kumuuliza maswali na kuyajibu kabla hajafungua maabara ya sayansi na maktaba na mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule hiyo. Wengine wanaoonekana ni wageni alioambatana nao na walimu wa Tusiime.

membe8

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa kidato cha pili sekondari ya Tusiime, Khadija Suleiman kuhusu namna ya kuchuja maji wakati Waziri alipofungua rasmi maabara ya kisasa ya sayansi na maktaba na mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule hiyo.

membe9

 

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akipata maelezo kutoka kwa Angela Shanira wa kitado cha tano sekondari ya Tusiime Tabata kuhusu masuala mbalimbali ya kisayansi kwenye maabara ya shule hiyo wakati Waziri alipofungua rasmi maabara ya kisasa ya sayansi na maktaba na mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule hiyo.

membe10

 

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akikata utepe kuzindia maabara ya kisasa ya sayansi na maktaba ya shule ya sekondari Tusiime kabla yajatoa vyeti kwa wahitimu wa kitado cha Sita wa shule hiyo. Wengine ni kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. John Mbogoma kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa shule hizo, Albert Katagira, Meneja wa shule Jane Katagira, na Mkuu wa shule ya sekondari Tusiime, Emil Rugambwa.