PSLE 2016 Examination Results – TUSIIME YAONGOZA KIWILAYA DARASA LA SABA

PSLE 2016 Examination Results – TUSIIME YAONGOZA KIWILAYA DARASA LA SABA

TUSIIME YAONGOZA TENA
SHULE ya Msingi Tusiime ya Dar es Salaam, imeendeleza umwamba kielimu kwa kushika nafasi ya tano kitaifa ikiwa na wanafunzi wengi kuliko shule zote zilizoingia kumi bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka huu ambapo ilikuwa na wanafunzi 210.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), Tusiime imefanikiwa kutoa mwanafunzi bora wa kwanza, wa pili na wa sita kitaifa kwa upande wa wasichana na mwanafunzi wa
wanne kwa upande wa wavulana walioingia kumi bora kitaifa.

Shule 4 zingine bora zote zikiwa na watahiniwa wasiozidi 50 ukilinganisha na Tusiime wakiwa na watahiniwa 210 ni

Mugini – watahiniwa 40
ROCKEN HILL – watahiniwa 50
KWEMA MODERN – watahiniwa 50
Fountain of Joy – watahiniwa 45.

Aidha, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na NECTA, wanafunzi wote 209 wa shule hiyo wamefaulu kwa wa daraja A na mmoja tu ndiye aliyepata B hivyo kuiwezesha shule hiyo kufaulu kwa wastani wa alama 227.8048

Kwa kifupi Shule ya Tusiime imefanya kama ifatavyo:
WALIOSAJILIWA : 210
WALIOFANYA MTIHANI : 210
WASTANI WA SHULE : 227.8048
KUNDI LA SHULE : Watahiniwa 40 au zaidi
NAFASI YA SHULE KWENYE KUNDI LAKE KIWILAYA: 1 kati ya 81
NAFASI YA SHULE KWENYE KUNDI LAKE KIMKOA : 2 kati ya 404
NAFASI YA SHULE KWENYE KUNDI LAKE KITAIFA : 5 kati ya 8109

209 wamepata wastani wa daraja A na 1 daraja B

psle-2016-full