SFNA 2015 ASSESSMENT RESULTS – PRIMARY 4

SFNA 2015 ASSESSMENT RESULTS – PRIMARY 4

SHULE ya Msingi Tusiime imeubeba Mkoa wa Dar es Salaam tena na kuwa Mkoa wa kwanza kitaifa katika matokeo ya darasa la nne mwaka huu baada ya shule hiyo kuingia kumi bora kitaifa ikiwa na idadi kubwa ya wanafunzi ( 248) idadi ambayo ni kubwa kuliko shule yoyote iliyoingia kumi bora.
Vile vile, matokeo hayo yameonyesha kwamba katika halmashauri kumi bora kitaifa, Wilaya ya Ilala ya jijini Dar es Salaam, imeongoza kwa kuwa ya kwanza kitaifa  kwa kupata asilimzia 99.45.
Tusiime imeingia kumi bora ikiwa na wanafunzi  248, idadi ambayo ni kubwa mara nne ya idadi ya wanafunzi wa  shule zote zilizoingia kumi bora ambapo shule nyingi zimeingia zikiwa na wanafunzi kati ya 40, 45, 52 na zingine zikiwa na wanafunzi 43.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), Tusiime ndiyo shule pekee ilifanikiwa kuingia kumi bora kitaifa Kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
Shule zingine zilizoingia kumi bora na idadi ya wanafunzi kwenye mabano ni  Alliance ya Mwanza (40), Waja Springs ya Geita (64), St Peter ya kagera (54), Tumaini ya Mwanza (43), Furaha Mwanza (52), Acacia Land Tabora (48), Imani ya Kilimanjaro (61),  Kaizirege Kagera (88) na Ebenezer ya Kilimanjaro (45).
Mkuu wa shule hiyo, Philbert Simon alishukuru kwa matokeo hayo mazuri na aliwaahidi wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo kuwa wamejipanga kusimamia  na kuendeleza mafanikio hayo ya shule za Tusiime.
“Kuingia kumi bora ukiwa na wanafunzi 248
haikuwa kazi rahisi ilibidi tufanye kazi kwa nguvu kweli kweli na utafiti wetu umeonyesha kuwa tangu mtihani wa darasa la nne uanze hakuna shule iliyowahi kuingia kumi bora kitaifa ikiwa na idadi kubwa ya wanafunzi kama hii ya Tusiime,” alisema.
Tusiime imekuwa ikiongoza Mkoa wa  Mkoa wa Dar es Salaam  kwa mtihani wa darasa la nne kwa miaka kumi mfululizo na kwenye matokeo ya kidato cha pili ya hivi karibuni asilimia 99 ya wanafunzi wa shule hiyo walifaulu kwa daraja la juu yaani ufaulu uliojipambanua (Distinction).
SFNA-2015