Shule ya Tusiime Yangara Tena Kidato Cha Pili

Shule ya Tusiime Yangara Tena Kidato Cha Pili

Baada ya kuongoza kwa kutoa wanafunzi bora kitaifa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana, shule ya sekondari ya Tusiime iliyoko Tabata, Dar es salaam imeendelea kung’ara kutoa wanafunzi bora kitaifa katika mmatokeo ya kidato cha pili mwaka huu. Mwanafunzi wa shule hiyo Antony Mataro, alipata alama ya juu zaidi ambayo ni 93 kwa kufanikiwa kufaulu katika masomo yote ambapo alipata alama kama ifuatavyo:

Physics : 100, Chemistry : 100, Mathematics : 95, Bookkeeping : 95, Biology : 91, English : 98, Geography : 96, History : 90,Civics : 91, Kiswahili : 76, Commerce : 84.

Matokeo yanaonyesha shule hiyo imeendelea kufanya vizuri ambapo kati ya wanafunzi 235 wa Tusiime, jumla ya wanafunzi 22 wamepata alama A wakati 152 wamepata alama B na wanafunzi 61 wamepata C. Katika matokeo hayo hakuna mwanafunzi hata mmoja aliyefeli mtihani huo wala aliyepata alama ya D au F.