STANDARD FOUR NATIONAL ASSESSMENT (SFNA) – 2016 RESULTS

STANDARD FOUR NATIONAL ASSESSMENT (SFNA) – 2016 RESULTS

Tusiime yatia fora, yaongoza tena Dar
Wanafunzi wote wapata daraja la kwanza na la pili.

SHULE za Tusiime zilizopo Tabata jijini Dar es Salaam, zimeendelea kufanya vizuri katika matokeo ya kitaifa ya darasa la nne ambapo kwenye matokeo hayo imeongoza tena kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kwenye matokeo yaliyotangazwa mwishoni mwa wiki na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), shule hiyo imeendelea kuvunja rekodi ya kuwa na ufaulu mzuri huku ikiwa na wanafunzi wengi na bila kuzingatia kigezo cha watoto wenye vipaji maalum.
Shule hiyo ikiwa na wanafunzi 230 wa darasa la nne, kati yao wanafunzi 226 wamepata ufaulu wa daraja A na wanne tu ndiyo wamepata daraja B.

Kwa kifupi Shule ya Tusiime imefanya kama ifatavyo:
WALIOSAJILIWA : 230
WALIOFANYA MTIHANI : 230
WASTANI WA SHULE : 272.7913
KUNDI LA SHULE : Watahiniwa 40 au zaidi
NAFASI YA SHULE KWENYE KUNDI LAKE KATIKA HALMASHAURI/MANISPAA: 1 kati ya 91
NAFASI YA SHULE KWENYE KUNDI LAKE KIMKOA : 1 kati ya 468
NAFASI YA SHULE KWENYE KUNDI LAKE KITAIFA : 11 kati ya 11025

SFNA-2016