MKOA wa Dar es Salaam umetangaza matokeo ya waliohitimu darasa la saba ya mwaka jana ambapo shule ya Tusiime ya Tabata jijini Dar es Salaam imeongoza kwa Mkoa wa Dar es Salam.
Shule hiyo ndiyo imekuwa ikiongoza matokeo ya mkoa na wilaya ya Ilala tangu mwaka 2005. Katika matokeo hayo wanafunzi 10 bora wa kike waliofanya vizuri wanatoka shule ya Tusiime kati ya wavulana walioingia 10 bora saba wanatoka shule hiyo.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mbando,aliwataja wanafunzi kumi bora wa kike wanaotoka katika shule ya Tusiime na alama zao kwenye mabano kuwa ni Janeth Kijazi (234), Justina Kalalaa (234, Kellen Mudogo (234), Thecla Ngewe (231), Stella Kagumila (230), Asia Komba (229), Grace Nyondo (226), Praise Bagenda (226), Lisa Magoti (225) na Najima Majid (224) (Tusiime).
Kwa upande wa wavulana 10 bora waliofanya vizuri na alama zao kwenye mabano ni Jimmy Luhomvya (233) Dule Mutagwaba (231), Fray Seyumwe (231) Saad Mussa (229) Gerald Kasamala (229), Oel Mutagwaba (228) na Gift Kilupa (229) ambao wote wanatoka shule ya Tusiime.
Wengine ni Maximillian Machage (229) kutoka Shule ya Msingi Kinondoni,Shaban Kawaia (227) Mtoni Temeke na Alfred Shami wa Shule ya Msingi Mlimani.